Breaking News

MWANADAMU UMEUMBWA KUSHINDA

Na Mwandishi Wetu | Arusha | Askofu wa Kanisa la ‘Christian Life Church’ Sinai Mlima wa Washindi lililopo Sakina jijini Arusha, Joseph Laizer amewaasa vijana waliohitimu katika vyuo mbalimbali nchini kuwa mwanadamu ameumbwa kushinda.


Askofu Laizer, Baba wa Washindi ameyasema hayo kwenye mahojiano maalum aliyoyafanya na mwandishi wetu jijini humo.

Vijana wengi huishia kulalama na kuiona serikali kama sio msaada kwao kisa kukosa namna ya kupata ajira mara tu ya wao kuhitimu elimu yao, huku wakisahau ile nafasi ya kupata elimu bure na ya mkopo vyuoni ni njia tosha ya kuwapelekea kwenye mafanikio wayatakayo

Wanadamu tumeumbwa washindi, sasa ili kufikia lengo la ushindi kuna vitu vya kufanya na sio kulalamika, na kubweteka, unahitajika kufanya mambo kwa zaidi ya vile ilivyozoeleka

Mchezaji bora kwenye mashindano ni Yule anayejituma na kufanya jambo la ziada ambalo litapelekea timu yake kushinda, na sio kulalama kutegemea huruma za mwamuzi wa mchezo” alisema Askofu Laizer.

Vijana wanasahau kuwa thamani ya maisha yao yapo ndani yao wenyewe, hakuna atakayekuthamini usipojithamini wewe mwenyewe

Wewe ni msomi leo, hakikisha hautembei jinsi ile wengine walitembea, maana unachokifanya leo ndio matokeo ya kesho yako, ukipanda malalamiko utavuna hay ohayo malalamiko, hakikisha unafanya kile wengine hawafanyi

Unataka kufanya biashara sawa, hakikisha unafanya zaidi na vile wengine wanafanya hapo ndipo utakapoona ushindi, siku zote tumeumbwa kushinda, hatukuumbwa kushindwa

Biblia mara kadhaa inatufundisha kuwa Mkono wa mwenye bidii Utatawala, ni waase vijana na watanzania kwa ujumla, serikali imetutengenezea jukwaa tayari la mafanikio, ni sisi ndio tunatakiwa kujipanga vizuri ni namba gani tunaiweza kuicheza kiufasaha na kwa ubora huku tukiongeza bidii na ubora kwenye kile tunachokitakakukifanya” aliongeza Askofu Laizer.

Kanisa la ‘Christian Life Church’ Sinai Mlima wa Washindi ni huduma inayopatikana katika jiji la Arusha maeneo ya Sakina, wengi wanapokea na kushuhudia ukuu wa kiungu kupitia Roho wake Mtakatifu.

No comments