UCHAGUZI KURA ZA MAONI MADIWANI WAFANYIKA KATA YA BUYUNI KIVULE
Na Mwandishi wetu
Uchaguzi kura za maoni ndani ya ccm umeendelea kushika kasi ambapo leo umeendelea kwa hatua kwa wanaoomba nafasi za udiwani.
Wilayani ilala katika kata ya buyuni bwana Karim Madenge ameongoza kwakupata kura 57 kati ya kura 160 kwenyemkutano mkuu wa kata hiyo.
Wajumbe 164 Leo tarehe25 julai 2020, wamemchagua Karim Madenge katika kura za maoni kwa mgombea wa nafasi ya Udiwani katika kata ya buyuni Ilala jiji Dar es Salaam kupitia tiketi ya Chama cha Mapnduzi CCM katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Msimamizi wa uchaguzi huo alimtangaza Jessica Motto kuwa mshindi wa pili kwakupata kura 37, huku anaefuata alieshika nafasi ya tatu alipata kura 22.
Ndugu wa jumbe wa mkutano huu wajumbe waliopiga kura ni 160 na wagombea jumala yao ni 22 hivyo tufuate kanuni za uchaguzi kisheria.
Akizungumza baada ya matokeo hayo msimamizi wa matokeo Juma Abdallah Mnambya aliseme kuwa mbali na matokeo yaliopatikana leo basi haimaanishi kuwa alieshinda leo kwenyekura za maoni ndio Diwani wa kata hiyo.
Amesema kuwa majina yote yatapelekwa kwa viongozi wa ngazi za juu ili kuyafanyia kazi ndio watarudisha jina la mmoja kati ya wagombea kwaajili ya kuingia kwenye uchaguzi mkuu hivyo nawaomba tusijengeane chuki tusipeanemaneno ya kebehi kikubwa tuendelee kushikamana ili kuendeleza jukumulakuongoza nchi yetu pamoja na chama chetu.
Uchaguzi huo uliofanyika katika kata hiyo huku kukiwa na dosari ndogondogo ikiwepo Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Nyeburu, Hamisi Mohamedi Gea kusababisha vurugu zilizoleta sintofahamu kwa wajumbe wa mkutano huo.
Mwenyekiti huyo alionesha utovu wa nidhamu katika uchaguzi huo mbele ya wasimamizi wa uchaguzi huo.
Baadhi ya wajumbe walikerwa sana na kitendo cha Mwenyekiti wa Nyeburu, Hamisi Mohamedi Gea kuleta vurugu katika uchaguzi wa amani na uwazi.
Kwa upande wake mshindi wa pili wa Kura za maoni ngazi ya udiwani Jessica Motto alisema yeye amepokea matokeo kama yalivyotangazwa.
Jessica alisema "Nashukuru kufikia hatua ya kwanza kura za maoni, pamoja na dosari zilizojitokeza mimi ni mwanachama kindakindaki wa Chama cha Mapinduzi (CCM), nimesikitishwa sana na vurugu ambazo kiongozi wetu wa ngazi ya Mwenyekiti Serikali ya Mtaa kufanya vurugu zile na kuwakosea heshima kamati ya siasa na wasimamizi toka ngazi ya juu Wilaya.Ni utovu wa nidhamu na hili liangaliwe kwa makini katika kuwasimamisha viongozi wa aina hii Kwaajili ya kulinda chama". alisema Motto.
Mwenyekiti wa CCM Kata ya Buyuni Jacob Nyajiego, wakati wa mkutano mkuu wa wajumbe kuchagua wagombea wa udiwani kata ya Buyuni iliyoko wilaya ya ilala jijini Dar es Salaam leo.
Jessica Motto ambae ameshika nafasi ya pili kura za maoni akijinadi kuomba kura kwa wajumbe wa mkutano huo
Jessica Motto ambae ameshika nafasi ya pili akihesabia kura zake
Vurugu za tokea uchaguzi kata ya Buyuni
No comments