UMOJA WA WANAWAKE KITUNDA WAFANYA ZIARA KUTEMBELEA WENYE UHITAJI MAALUM
Afisa Maendeleo kata ya Kitunda, Sosina Soka (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open
Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna Haule pamoja na Wanachama wa Umoja wa
Wanawake wa Kata ya Kitunda akikabidhi msaada wa taulo za wasichana kwa wasichana waliopo
katika kituo cha Kulea watoto yatima pamoja na wanaoishi katika mazingira
magumu cha Camp Caleb katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya
wanawake duniani ambayo kwa kata ya Kitunda yatafanyika tarehe 7 machi katika
viwanja vya shule ya msingi Kerezange.
Baadhi ya Wanachama wa Umoja wa Wanawake wa Kata
ya Kitunda wakikabidhi msaada wa godoro, unga na sukari kwa Mmoja wa wakazi wa kata
hiyo mwenye mazingira magumu kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
yatakayofanyika tarehe 8 machi. Umoja huo umefanya hafla ya kuwatembelea watu
wenye uhitaji mbalimbali pamoja na kutembelea kituo cha watoto yatima cha Camp
Caleb kilichopo mtaa wa Kipera kata ya Kitunda.
Matembezi hayo yamefanyika jijini Dar es Salaan jana.
Umoja wa Wanawake wa Kata ya Kitunda wakiongozana
kwa pamoja wakiwa na misaada yao kueleka kwa watu wenye uhitaji katika
kuadhimisha siku ya wanawake duniani. Ni miongoni wa mwa mila na desturi za
umoja huo kusaidia wenye uhitaji maalum. Matembezi hayo yamefanyika jijini Dar
es Salaan jana.
Baadhi ya Wanawake wa Umoja wa Wanawake wa Kata
ya Kitunda wakisalimiana na Mmoja wa wakazi wa Kitunda, Bibi Tausi Ramadhani
baada ya kuwasili mahali alipohifadhiwa kwaajili ya kumkabidhi msaada katika
kuadhimisha siku ya wanawake duniani.
Umoja wa Wanawake wa Kata ya Kitunda wakikabidhi
msaada wao kwa Bibi Tausi Ramadhani katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya
siku ya wanawake duniani ambayo kwa kata ya Kitunda yanafanyika tarehe 7 machi
katika viwanja vya shule ya msingi Kerezange.
Umoja wa Wanawake wa Kata ya Kitunda wakikabidhi msaada wao kwa Mwakilishi wa Bibi anayeishi katika mazingira Magumu Bibi Salum katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kwa kata ya Kitunda yanafanyika tarehe 7 machi katika viwanja vya shule ya msingi Kerezange.
Mwanachama wa Umoja wa Wanawake wa Kata ya
Kitunda akizungumza jambo na watoto yatima pamoja na wanaishi katika mazingira
magumu baada ya kuwasili katika kituo cha Kulea watoto hao cha Camp Caleb
kilichopo katika mtaa wa Kipera kata ya Kitunda kwa ajili ya kutoa msaada
katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kwa
kata ya Kitunda yatafanyika tarehe 7 machi katika viwanja vya shule ya msingi
Kerezange.
Baadhi ya Wanachama wa Umoja wa Wanawake wa Kata
ya Kitunda wakiimba nyimbo za kukataa unyanyasaji wa kijinsia baada ya kuwasili
katika kituo cha Kulea watoto yatima pamoja na wanaoishi katika mazingira
magumu cha Camp Caleb kilichopo katika mtaa wa Kipera kata ya Kitunda kwa ajili
ya kukabidhi msaada katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya wanawake
duniani.
Afisa Maendeleo kata ya Kitunda, Sosina Soka
akigawa biskuti kwa watoto wanaolelewa
katika kituo hicho.
Wanachama wa Umoja wa Wanawake wa Kata ya Kitunda wakiwa katika picha ya
pamoja na watoto wanaolelewa katika kituo cha Kulea watoto yatima pamoja na
wanaoishi katika mazingira magumu cha Camp Caleb katika kuelekea kilele cha
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kwa kata ya Kitunda yatafanyika
tarehe 7 machi katika viwanja vya shule ya msingi Kerezange.
Afisa Maendeleo kata ya Kitunda, Sosina Soka (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Taasis ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open
Mind and Thoughts Organization (OMTO), pamoja na Wanachama wa Umoja wa
Wanawake wa Kata ya Kitunda msaada wa chandarua kwa watoto waliopo katika kituo
cha Kulea watoto yatima pamoja na wanaoishi katika mazingira magumu cha Camp
Caleb katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo
kwa kata ya Kitunda yatafanyika tarehe 7 machi katika viwanja vya shule ya
msingi Kerezange.
HABARI KATIKA PICHA
Heri ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
No comments