Breaking News

FAINALI ZA PROPHET SUGUYE CUP ZAFANA

Mashindano ya mpira wa miguu yaliyopewa jina la Prophet Suguye Cup ambayo yalikuwa yanatimua vumbi katika viwanja vya Shule ya Msingi Misitu iliyopo Kivule, Ukonga, Dar es Salaam na kudhaminiwa na Muasisi wa Mashindano hayo Nabii Nicolaus Suguye wa Kanisa la WRM lenye Makao yake Makuu Kivule matembele ya Pili, Ukonga, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa mshindi wa mashindano hayo, muasisi wa mashindano hayo Nabii Nicolaus Suguye amesema lengo la Mashindano hayo ni kuwaweka pamoja na kuwahamasisha vijana kufanya kazi ili kuwasaidia kukwepa maovu yatokanayo na kukaa vijiweni bila shughuli maalumu.

Mashindano hayo yalianza kutimua vumbi tarehe 25 Mei 2019 na kufikia tamati hapo jumamosi ya tarehe 10 Agosti 2019 kwa timu ya FAIRPLAY kuibuka wafalme wa kwanza wa mashindano hayo yaliyoshirikisha timu 24 kutoka maeneo yanayounganisha jimbo la Ukonga wilayani Ilala, Dar es Salaam.

Timu ya FAIRPLAY ya KIVULE jijini DAR ES SALAAM imeibuka kidedea na kuchukua ubingwa wa mashindano hayo baada ya kuichabanga timu ya KIVULE FOREST kwa jumla ya bao mbili kwa moja, katika fainali ya ligi ya mpira wa miguu ya PROPHET SUGUYE CUP.

Mshambuliaji wa timu ya Fair Play FC, akijaribu kuwatoka mabeki wa  Kivule Forest FC, wakati wa mchezo wa Fainali Ligi ya Prophet  Suguye Cup iliyokuwa ikiendelea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Misitu Kivule nje kidogo ya Jiji la DaresSalaam ambapo Fair Play iliibuka kidedea kwa mabao 2-1, nakufanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika mchezo huo nakukabidhiwa kombe na Mwanzilishi wa ligi hiyo Nabii Nicolaus Suguye wa kanisa la WRM.
Nahodha wa Fair Play akipokea kombe kutoka kwa Mwanzilishi wa ligi hiyo Nabii Nicolaus Suguye wa kanisa la WRM baada ya kuibuka na ushindi wakati wa mchezo wa Fainali katika mchezo wa Ligi ya Prophet Suguye Cup iliyokuwa ikiendelea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Misitu Kivule, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo ambapo Fair Play iliibuka kidedea kwa mabao 2-1. Nakufanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika   Mchezo huo nakukabidhiwa kombe na Mwanzilishi wa ligi hiyo Nabii Nichoraus Suguye wa kanisa la WRM lililopo Kivule Matembele ya pili, Mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Nahodha wa Kivule Forest FC, Jolvin Balotel akipokea kombe kutoka kwa Nabii wa Kanisa la UKOMBOZI MINISTRIES FOR ALL NATIONS-BG.MALISA baada ya kushika nafasi ya pili wakati wa mchezo wa Fainali Ligi ya Prophet Suguye Cup iliyokuwa ikiendelea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Misitu Kivule, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo Fair Play iliibuka kidedea kwa mabao 2-1. Nakufanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika Mchezo huo.
Nahodha wa Kivule FC akionesha kombe baada yakukabidhiwa.
Wachezaji wa timu hizo wakiwania mpira wakati wa mchezo wa fainali.
Wachezaji wa Fairplay FC wakifurahia baada yakukabidhiwa kombe na Nabii Nicolaus Suguye wa Kanisa la WRM na Muanzilishi wa ligi hiyo, wakati wa mchezo wa fainali katika mchezo wa Ligi ya Prophet  Suguye Cup iliyokuwa ikiendelea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Misitu Kivule, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo Fair Play iliibuka kidedea kwa mabao 2-1. Nakufanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika Mchezo huo nakukabidhiwa kombe na Mwanzilishi wa ligi hiyo Nabii Nicolaus Suguye.

No comments