Breaking News

RC Makonda akoshwa na Kasi ya ujenzi wa Miradi mbalimbali Katika Wilaya ya Kinondoni


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda(Katikati) Pamoja na watendaji wa Wilaya ya Kinondoni wakiwa Katika Ziara ya Ukaguzi wa miradi mbalimbali Katika Wilaya hiyo.


 RC Makonda akikagua mitaro ya maji inayojenga Tandale 






 Baadhi ya mafundi wakiendelea na Ujenzi wa Soko la Magomeni Usalama Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es Paul Makonda amefurahishwa na Kasi ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo Katika Wilaya ya kinondoni ambapo mpaka kufikia Sasa utekelezaji wake unaenda vizuri.

Ikiwa Ni mwendelezo wa Ziara yake, Leo April 15, RC Makonda ametembelea miradi mbalimbali Katika Manispaa ya Kinondoni ambapo lengo la Ziara hiyo Ni kuona Kasi ya utekelezwaji wa ujenzi Katika miradi hiyo ambayo ni miradi Katika sekta ya Afya, Barabara ambayo imetolewa fedha kutoka Katika Serikali.


RC  Makonda ametembelea ujenzi wa Soko la Magomeni,ujenzi wa kituo Cha Afya kigogo ambao unatarajiwa kukamilika hivi karibunii, Soko la Sinza, Pamoja na ujenzi wa Barabara ya Barafu Mbulahati,  ambapo amewataka wakandarasi kufanya kazi zao kwa kuzingatia ueledi.

Amesema wakandarasi wamekuwa wakifanya kazi bila kuzingatia viwango Jambo linalopelekea barabara kuwa mbovu baada ya muda mchache, ambapo amesema wapo waliofungiwa kufanya kazi Katika mkoa huo, na wengine kutakiwa kurudia ujenzi wa barabara kwa fedha zao wenyewe.


Aidha amemtaka Mkuu wa Wilaya ya hiyo kuhakikisha anaendelea kusimamia kikamilifu miradi yote ili iweze kukamilika kwa wakati uliopangwa na kuweza kutatua kero na adha zinazowakumba wananchi.

Pia amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kushughulikia changamoto za malipo kwa wa Vibarua rwanaofanya kazi katika miradi hiyo huku akiweka sawa mailpo halali wanayotakiwa kulipwa kuwa ni kiasi cha shilingi 12,500 na si chini na hapo.
“Tuna matumaini makubwa sana kutokana na kasi wanayoenda nayo na nampongeza sana DC kwa kazi anayoifanya, barabara ya kituo cha simu 2000 pia inaendelea vizuri na kuna kipande cha mita 250 kimechukuliwa na TANROADS kwa jailli ya kuunganisha na ujenzi wa barabara ya Ubungo hivyo wananchi wakiona kinachelewa wasijiulize kwa Nini hii Ni kwamba tunataka kuunganisha na ujenzi wa barabara ya juu inayojengwa ya Ubungo" Amesema Rc Makonda.
Ziara ya kukagua miradi ndani ya Mkoa huo bado zinaendelea ambapo siku ya kesho RC Makonda ataendelea na ziara katika wilaya ya Kinondoni

No comments