KATA ZA JIMBO LA UKONGA ZANUFAIKA NA PESA ZA MFUKO WA JIMBO
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (wapili kushoto) akizungumza na
Viongozi wa Kata za Jimbo hilo pamoja na Wananchi jijini Dar es Salaam leo wakati
wa Kikao cha kukabidhi mashine 5 za kutolea kopi (Printer) zenye thamani ya
Shilingi Milioni 25 kutoka katika fedha ya Mfuko wa Jimbo la Ukonga.Waitara
amekabidhi mashine hizo kwa kata 5 ambazo ni, Pugu Station, Buyuni, Chanika,
Msongola na Zingiziwa ambapo Kata zilizobakia zitapata kwa awamu ijayo ya fedha
ya Mfuko wa Jimbo hivyo basi Mbunge ameanza kukabidhi mashine hizo kwa kata
ambazo zenye uhitaji zaidi.Vilevile Waitara amekabidhi Jezi pamoja na Mipira
kwa Viongozi wa Kata zote 13 zilizopo Jimbo la Ukonga kwa Lengo la kuanzisha
Ligi ndani ya kata ili Mradi washindi watakaopatikana wataingia kwenye Ligi
kubwa ya Jimbo ambayo itatoa Timu ya
Jimbo la Ukonga.Kutoka kushoto ni Katibu Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Ilala, Said
Sidde, Mwenyekiti wa CCM kata ya Pugu, Bilungo Mangara, Mchumi wa Manispaa pia
ni Katibu wa Mfuko wa Jimbo la Ukonga, Mpossi Gwakisa na Afisa Elimu Shule za
Sekondari Manispaa ya Ilala, Eliza Ngonyani.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (kushoto) akikabidhi Mashine za
kutolea kopi (Printer) kwa Viongozi wa Kata za Pugu Station, Buyuni, Chanika,
Msongola na Zingiziwa.
Vilevile Mfuko wa Jimbo
umegawanywa kama ifuatavyo,Ununuzi wa Tanki la lita 5000 kwa kikundi cha Waosha
magari Guluka Kwalala kata ya Gongo la Mboto Shilingi 3,000,000/= ,Kikundi cha ULIDA kata ya
Kivule sh.5,000,000/= , Ununuzi wa Kompyuta 1 Shule ya Sekondari Kitunda
Sh.1,000,000/= , Ujenzi wa Kalavati eneo la Nyeburu Magombeni kata ya Buyuni
Sh.10,000,000/= , Ujenzi wa Kalavati Zingiziwa Sh.5,000,000/= , Ukarabati wa
matundu ya choo Shule ya Sekondari Chanika kata ya Zingiziwa Sh.1,000,000/= ,
Ukarabati wa Shule ya Sekondari Zingiziwa Sh.1,000,000/= ,
Ujenzi wa Kivuko cha
Mavuno kata ya Gongo la Mboto Sh.4,000,000/= ,Ununuzi wa mabomba ya kusambaza
maji eneo la Pugu Stesheni (watumia maji) Sh.5,000,000/= , Uchangiaji wa Ujenzi
wa Ofisi ya serikali ya Mtaa Kerezange kata ya Kivule Sh.5,000,000/= ,
Usafishaji kisima cha maji na usambazaji wa maji Ulongoni “B’’ kata ya Gongo la
Mboto Sh.3,000,000/= ,
Ununuzi wa mipira Waitara
Cup Jimbo la Ukonga Sh.2,000,000/= , Gharama za kukodisha gari kusambaza kifusi
katika barabara za kipunguni “B’’ Sh.1,000,000/= pamoja na Ununuzi wa Mashine
za Kutoa Kopi (Printer) 5 kwa kata za Pugu Station, Buyuni, Chanika, Msongola
na Zingiziwa Sh.25,000,000/= jumla yake ni Shilingi Milioni 71.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (kushoto) akikabidhi Jezi
pamoja na Mipira kwa Viongozi wa Kata zote 13 zilizopo katika jimbo hilo jijini
Dar es Salaam leo kwa lengo la kuanzisha Ligi za kata ambazo washindi wataingia
kwenye ligi ya Jimbo ambayo itatoa Timu ya Jimbo la Ukonga.
Baadhi ya Viongozi wa Kata zote za Jimbo la Ukonga pamoja na wakazi wake
wakimsililiza kwa makini Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara wakati wa
kikao cha kukabidhi mashine 5 za kutolea kopi (Printer) kikiendelea.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mbaraka Mwinyi akizungumza katika
hafla hiyo.
Katibu Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Ilala, Said Sidde akitoa shukrani
za dhati kwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga baada ya kukabidhi mashine 5 za kutolea
kopi (Printer) pamoja na vifaa vya michezo.
No comments